MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPA


RATIBA YA ROBO FAINALI CAF CHAMPIONS LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPARATIBA YA NUSU FAINALI CAF CHAMPIONS LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPA


RATIBA YA SIMBA ROBO FAINALI CAF CHAMPIONS LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPA


RATIBA YA YANGA ROBO FAINALI CAF CHAMPIONS LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPA


ASANTE na Kwaheri MUHALILA CUP 2023

Filed in Michezo by on 31/12/2023 0 Comments

ASANTE na Kwaheri MUHALILA CUP 2023

ASANTE na Kwaheri MUHALILA CUP 2023

ASANTE na Kwaheri MUHALILA CUP 2023

ASANTE na Kwaheri MUHALILA CUP 2023,”Kila lenye mwanzo lina mwisho ” sauti hii na mwangwi mkubwa vilisikika kutoka kwenye mgongo wa ardhi ya BUHAYA tarehe naikumbuka ni 18 Novemba, 2023.

Gwiji na mdau wa soka Ulimwenguni akatua kwa mara ya kwanza kwenye viunga vya KAGOMA akayafungua Mashindano na akaziacha Neema nyingi na akaondoka zake, tukio la kukumbukwa na wapenda kandanda wa kata Kagoma, Kikuku na Majirani zake Asante Digala SAFFIH DAUDA KAJUNA.

Tumeshuhudia jumla ya timu 16 zikichuana katika msimu wa 2023 kwa majina nakupa hii chukua na ubaki nayo (Ndangala, Kikuku, Ihumbo, Chipukizi Boys, Manyora, Itoju, Muleba Stars, Ngenge Combine, Mijure, Burigi, New MBN, Muyenje, Nsisha, Kamachumu, Butembo na Ntungamo.

Ligi ilichezwa kwa hatua ya Makundi na tukashuhudia timu 8 zikivuka kwenda hatua ya Robo Fainali (Ndangala, Burigi, Kikuku, Mijure, Manyora, Kamachumu, Nsisha na Itoju.

Nusu Fainali ikawa suprise kwa baadhi ya timu zenye mashabiki wengi na majina makubwa kwa historia katika mashindano, ni timu 4 pekee zilipata nafasi (Ndangala, Itoju, Kikuku na Kamachumu) katika timu hizi 4 ni Kikuku pekee ambaye ni mkongwe katika mashindano.

Leo tarehe 31-12-2023 Dunia itashuhudia kwa mara nyingine Kagoma ikisimama kwa dakika 90 kushuhudia mechi ya funga mwaka ikiwa FAINALI ya Muhalila Cup 2023, ndio ni KIKUKU FC dhidi ya ITOJU FC.

Saida Karoli ndani ya MUHALILA CUP 2023

Saida Karoli ndani ya MUHALILA CUP 2023

Fainali itapambwa kwa burudani yenye ladha ya BUHAYA kutoka kwa nguli na Bingwa wa mziki wa asili wenye vionjo vya kimataifa si mwingine bali ni SAIDA KAROLI.

ADV.Simon Patrick Ndani ya MUHALILA CUP 2023

ADV.Simon Patrick Ndani ya MUHALILA CUP 2023

Mgeni rasmi kwa heshima kubwa ni ADV.SIMON PATRICK Mwanasheria wa YANGA SC ambaye pia FIFA humtumia katika masuala ya kisheria, na amekuwa akifanya kazi kwa nyakati rofauti kwenye mahakama za kimataifa.

Tulianza pamoja na tunamaliza pamoja shukrani zetu ni kwa Mungu mwingi wa rehema.

Karibu Kagoma kuanzia majira ya saa 9:00 tujumuike pamoja kuyafunga Mashindano kwa namna ya kipekee.

Aidha Zawadi ya Bingwa wa Muhalila Cup msimu huu wa 2022/2023 itakuwa Tsh 2,000,000 na Mshindi wa Pili atajipatia kiasi Cha Tsh 1,000,000, huku Mshindi akiondoka na Tsh 500,000.

Timu Shiriki Muhalila Cup 2023/2024

 1. Kikuku FC
 2. Chipukizi Boys
 3. Ndangala FC
 4. Ihumbo FC
 5. Manyora FC
 6. Muleba Stars
 7. Itoju FC
 8. Ngenge Combaine FC
 9. Muyenje FC
 10. New MBN FC
 11. Burigi FC
 12. Mijure FC
 13. Nsisha FC
 14. Butembo FC
 15. Kamachumu Stars
 16. Ntungamo FC

Uwepo wa Mashindano ya Muhalila Cup kwa miaka tisa mfululizo yameitangaza Wilaya ya Muleba na Mkoa wa Kagera kwa ujumla na baadhi ya Vijana waliopitia Mashindano hayo wanacheza katika Ligi Kuu ya Tanzania (NBC Premier League?

PIA UNAWEZA KUSOMA👇

Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Nijuze Habari WhatsAp Channel
  Nijuze Habari WhatsAp Group
  Nijuze Habari Telegram Channel