NIDA inatoa vitambulisho vya aina tatu, ambavyo ni kitambulisho cha raia, kitambulisho cha mgeni mkaazi, na kitambulisho cha mkimbizi mwenye umri wa miaka 18 na kuendelea na anayeishi nchini kihalali.

i. Kitambulisho cha Raia

ciizen-id

Mahitaji yake:

 1. Cheti cha kuzaliwa
 2. Cheti za elimu ya msingi,
 3. Pasi ya kusafiria (Pasipoti)
 4. Cheti cha elimu ya sekondari (kidato cha iv na vi)
 5. leseni ya udereva
 6. Kadi ya bima ya afya
 7. Kadi ya mfuko wa hifadhi ya jamii
 8. Kadi ya mpiga kura
 9. Nambari ya mlipa kodi (Tin. No)
 10. Kitambulisho cha mzanzibar mkazi
 11. Barua kutoka kwa Mwenyekiti wa serikali ya mtaa

ii. Kitambulisho cha Mgeni Mkazi

Tanzania_LEGALRESIDENT_

Mahitaji yake:

 1. Pasport ya nchi anakotoka
 2. Kibali cha kukaa nchini kuendesha shughuli mbali mbali anazofanya mwombaji

iii. Kitambulisho cha Mkimbizi

Tanzania_REFUGEE_

Mahitaji:

 1. Hari ya Mkimbizi: Hati inayosibitisha kuwa mwombaji ana hadhi ya kuwa mkimbizi nchini