MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPA


RATIBA YA ROBO FAINALI CAF CHAMPIONS LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPARATIBA YA NUSU FAINALI CAF CHAMPIONS LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPA


RATIBA YA SIMBA ROBO FAINALI CAF CHAMPIONS LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPA


RATIBA YA YANGA ROBO FAINALI CAF CHAMPIONS LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPA


HESLB Mwongozo wa Utoaji Mikopo Toleo la Pili 2023/2024

Filed in Makala, Ajira, Michezo by on 11/03/2024 0 Comments

HESLB Mwongozo wa Utoaji Mikopo Toleo la Pili 2023/2024

HESLB Mwongozo wa Utoaji Mikopo Toleo la Pili 2023/2024, Mwongozo wa kuomba mkopo diploma, Mfano Wa Fomu Ya Mkopo HESLB PDF, Fomu Ya Kuomba Mkopo HESLB,Vigezo vya Kupata Mkopo ngazi ya diploma PDF Download, mwongozo wa utoaji mikopo 2023/2024, Mwongozo wa kuomba mkopo vyuo vya kati, Vigezo vya Kupata Mkopo HESLB dirisha la mkopo 2023/2024, Gpa ya kupata mkopo, Jinsi ya kuomba mkopo Online Mkopo kwa wanafunzi wa diploma, mwongozo wa kuomba mkopo 2023/24 pdf

HESLB Mwongozo wa Utoaji Mikopo Toleo la Pili 2023/2024

HESLB Mwongozo wa Utoaji Mikopo Toleo la Pili 2023/2024,Mwongozo Uombaji Mkopo kwa Diploma (2) 2023/2024,HESLB login, Bodi ya Mikopo Tanzania Login, Bodi ya mikopo Dodoma
SIPA HESLB login account, Bodi ya mikopo Zanzibar, HESLB Login as Registered User.

1.0 MAELEKEZO MUHIMU KWA WANAFUNZI WOTE WANAOOMBA MIKOPO

Waombaji wote wa mikopo ya
elimu kwa ngazi ya Stashahada kwa mwaka wa masomo 2023/2024 wanafahamishwa kuzingatia mambo
yafuatayo:-

 • Kusoma na kufuata taratibu za maombi katika Mwongozo
  wa mwaka wa masomo 2023/2024;
 • Kuhakikisha kuwa namba ya mtihani wa kidato cha nne
  atakayoitumia mwombaji iwe sawa na aliyoombea udahili
  wa chuo;
 • Kuhakikisha kuwa fomu ya maombi ya mkopo na mkataba
  zimesainiwa na viongozi wa serikali ya mtaa, mdhamini na
  kamishna wa viapo.;
 • Waombaji wajaze fomu zao kwa ukamilifu na kuzisaini kabla
  ya kuziwasilisha HESLB kwa njia ya mtandao;
  Kuhakikisha kwamba vyeti vya kuzaliwa/vifo vimethibitishwa
  na Wakala w Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) au Wakala wa
  Usajili wa Matukio ya Kijamii Zanzibar (ZCSRA) au Afisa
  aliyeteuliwa ili kuthibitisha uhalali wa nyaraka hizo;
 • Kwa mwombaji mwenye akaunti ya benki ajaze taarifa zake
  kwa usahihi kwenye fomu ya maombi ya mkopo;
 • Kwa mwombaji mwenye Namba ya simu na kitambulisho
  cha taifa (NIDA) ahakikishe anajaza namba hizo wakati wa
  kuomba mkopo.
 • Waombaji wote wanakumbushwa kuzingatia muda wa
  mwisho wa kutuma maombi kwa njia ya mtandao.

2.0 KUFUNGULIWA DIRISHA LA MAOMBI AWAMU YA PILI

Kwa wanafunzi wanaotarajia kuomba mikopo ya elimu kwa ngazi ya
Stashahada kwa awamu ya pili, dirisha la maombi ya mkopo kwa mwaka wa masomo 2023/2024 limefunguliwa kwa siku 14 kuanzia tarehe 21 Disemba, 2023 hadi tarehe 04 Januari, 2024.

Dirisha la awamu ya pili, wanafunzi walengwa wamegawanyika katika
makundi matatu ambao watapaswa kuwasilisha maombi yao kwa
njia ya mtandao kupitia https://olas.heslb.go.tz

Kundi la Kwanza ni wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Stashahada
za kipaumbele kama zilivyotajwa katika ‘TOLEO LA KWANZA’ la ‘Mwongozo wa Utoaji Mikopo ya Elimu kwa Wanafunzi wa Stashahada kwa mwaka 2023-2024’ ambao awali hawakuweza kuomba kwa
sababu mbalimbali ikiwemo kuchelewa hadi dirisha kufungwa.

Kundi la Pili ni wanafunzi wa mwaka wa pili au wa tatu wa Stashahada
za kipaumbele kama zilivyotajwa katika ‘TOLEO LA KWANZA’ la ‘Mwongozo wa Utoaji Mikopo ya Elimu kwa Wanafunzi wa Stashahada kwa mwaka 2023-2024’. Wanafunzi hawa, ambao awali hawakuweza kuomba mkopo, sasa wanaruhusiwa kuomba.

Kundi la Tatu ni wanafunzi wa Stashahada za kipaumbele ZILIZOONGEZWA kupitia mwongozo huu; ‘TOLEO LA PILI’ la ‘Mwongozo
wa Utoaji Mikopo ya Elimu kwa Wanafunzi wa Stashahada kwa mwaka
2023-2024’.

Wanafunzi wote wanaoomba mkopo wa Stashahada kupitia dirisha
hili la awamu ya pili wanakumbushwa kusoma ‘TOLEO LA KWANZA’ la
‘Mwongozo wa Utoaji Mikopo ya Elimu kwa Wanafunzi wa Stashahada
kwa mwaka 2023-2024’ ambao unapatikana katika www.heslb.go.tz
na www.nactvet.go.tz

3.0 SIFA STAHIKI

3.1 VIGEZO VYA MSINGI VYA MWOMBAJI MKOPO

Sheria na Kanuni za Bodi ya Mikopo zinaainisha sifa na vigezo
vya jumla kwa wanafunzi wanaohitaji mkopo baada ya kudahiliwa na vyuo vyenye ithibati.

Mwombaji atatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:-

 • Awe Mtanzania mwenye umri usiozidi miaka 27 wakati
  wa kuomba mkopo;
 • Awe amedahiliwa katika taasisi ya elimu inayotoa elimu
  ya ngazi ya kati nchini;
 • Awe amekamilisha na kuwasilisha maombi ya mkopo
  kupitia mfumo wa maombi ya mkopo (OLAMS);
 • Asiwe na ajira au mkataba wa kazi wa serikalini au sekta
  binafsi unaompatia mshahara au kipato;
 • Awe amehitimu elimu ya kidato cha nne (CSEE), Cheti (astashahada) au kidato cha sita (ACSEE) au ndani ya
  miaka mitano; yaani kati ya mwaka 2019 hadi 2023.
 • RITA Utaratibu na Muongozo wa Kuhakiki Vyeti HESLB

3.2 HALI YA KIJAMII NA KIUCHUMI

 • Uyatima; aliyefiwa na mzazi au wazazi
 • Familia au kaya ya kipato duni inayofadhiliwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) au taasisi nyingine za kitaifa zinazotoa ufadhili kwa kaya zenye vipato duni;
 • Ulemavu wa mwombaji au wazazi wake.

4.0 UPANGAJI WA MIKOPO

Upangaji wa mikopo utazingatia
vipaumbele vifuatavyo:-

 • Mwanafunzi mwenye udahili kwenye programu za vipaumbele vya Taifa kama zilivyofafanuliwa katika Kipengele cha 6 cha Mwongozo huu zitazingatiwa;
 • Ufaulu wa kitaaluma uliomuwezesha kudahiliwa kwa ajili ya elimu ya ngazi ya
  kati; na
 • Hali ya kijamii kama ilivyofafanuliwa katika kipengele cha 3.2 cha mwongozo huu.

5.0 NYARAKA ZA KUAMBATISHA WAKATI WA MAOMBI YA MKOPO

Zifuatazo ni nyaraka muhimu za kuambatisha kwenye maombi ya
mkopo: –

 • Cheti cha kuzaliwa kutoka mamlaka husika, ZCSRA kwa
  waombaji kutoka Zanzibar au namba ya uhakiki (verification number) kutoka RITA kwa waombaji kutoka Tanzania Bara;
 • Vyeti vya vifo vya wazazi kuthibitisha uyatima kutoka
  mamlaka husika, ZCSRA kwa waombaji kutoka Zanzibar
  au namba ya uhakiki (verification number) kutoka RITA kwa waombaji kutoka Tanzania Bara;
 • Fomu ya kuthibitisha Ulemavu wa mwombaji au mzazi iliyoidhinishwa na Mganga Mkuu wa Wilaya (DMO) au Mkoa (RMO);
 • Fomu ya kuthibitisha Ulemavu wa mzazi wa mwombaji iliyoidhinishwa na Mganga Mkuu wa Wilaya (DMO) au Mganga Mkuu wa Mkoa (RMO);
 • Namba ya kaya ya Mnufaika kutoka kwenye Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).

HESLB Mwongozo wa Utoaji Mikopo Toleo la Pili 2023/2024, Mwongozo wa kuomba mkopo diploma, Mfano Wa Fomu Ya Mkopo HESLB PDF, Fomu Ya Kuomba Mkopo HESLB, Vigezo vya Kupata Mkopo ngazi ya diploma PDF Download, mwongozo wa utoaji mikopo 2023/2024, Mwongozo wa kuomba mkopo vyuo vya kati, Vigezo vya Kupata Mkopo HESLB dirisha la mkopo 2023/2024, Gpa ya kupata mkopo, Jinsi ya kuomba mkopo Online Mkopo kwa wanafunzi wa diploma, mwongozo wa kuomba mkopo 2023/24 pdf6.0 MAENEO NA PROGRAMU ZA
KIPAUMBELE KATIKA UTOAJI WA MIKOPO

6.1 MAENEO YA KIPAUMBELE

Mkopo utatolewa katika maeneo makuu sita yakiakisi vipaumbele vya Taifa kama ilivyoainishwa katika tangazo la
Serikali Namba 715 la tarehe 29 Septemba 2023.

Maeneo hayo ni kama ifuatavyo:-

 • ‘Health & Allied Sciences’;
 • ‘Education and Teaching’;
 • ‘Transport & Logistics’;
 • ‘Energy Engineering’;
 • ‘Mining & Earth Science’ and
 • ‘Agriculture & livestock’

6.2 PROGRAMU ZA KIPAUMBELE

Katika mwaka wa masomo 2023/2024 mikopo itatolewa kwa wanafunzi waliodahiliwa katika Program/Stashahada zinazoangukia/zilizomo katika maeneo sita ya kipaumbele yaliyoidhinishwa – rejea kipengele 6.

6.2.1 AFYA NA SAYANSI SHIRIKISHI
(HEALTH & ALLIED SCIENCES)

Programu katika kundi hili ni kama zifuatazo:-

 • ‘Clinical Dentistry’;
 • ‘Diagnostic Radiotherapy’;
 • ‘Occupational Therapy’;
 • ‘Physiotherapy’;
 • ‘Clinical optometry’;
 • ‘Dental Laboratory technology’;
 • ‘Orthotics & Prosthetics’;
 • ‘Health record & information; and
 • ‘Electrical and Biomedical Engineering’.

6.2.2 ELIMU YA UALIMU (EDUCATION AND TEACHING)

PROGRAMU KATIKA KUNDI HILI NI KAMA ZIFUTAZO:-

 • Diploma in Education (Physics and
  Mathematics); and
 • Diploma in Teaching (Technical and
  Vocational Education).

6.2.3 USAFIRI NA USAFIRISHAJI (‘TRANSPORT AND LOGISTICS’)

PROGRAMU KATIKA KUNDI HILI NI KAMA ZIFUATAZO:-

 • ‘Aircraft Mechanics’;
 • ‘Shipbuilding and repair’;
 • ‘Railway construction and maintenance;
 • ‘Global Logistics and Supply Chain
  Management’,
 • ‘Marine Trasport and Nautical Science’,
 • ‘Shipping and Logistics Management’, and
 • ‘Transport and Supply Chain Management’.

6.2.4 UHANDISI WA NISHATI (‘ENERGY ENGINEERING’)

PROGRAMU KATIKA KUNDI HILI NI KAMA ZIFUATAZO:-

 • ‘Renewable Energy Engineering
  (Hydro, Wind, Solar)’;
 • ‘Pipeline, Oil and Gas Engineering’,
 • ‘Oil and Gas Engineering Technology’,
 • Environmental Engineering and
  Management’,
 • ‘Naval Architecture and Offshore
  Engineering’,
 • ‘Metallurgy and Mineral Processing
  Engineering’, and
 • ‘Mining Engineering’.

6.2.5 MADINI NA SAYANSI YA ARDHI
(‘MINING AND EARTH SCIENCE’)

Programu katika kundi hili ni kama zifuatazo:-

 • ‘Lapidary and Jewelry’;
 • ‘Mineral Processing’,
 • “Geology and Mineral Exploration’,
 • ‘Petroleum Geosciences and Exploration’, and
 • ‘Land and Mine Surveying’.

6.2.6 KILIMO NA UFUGAJI (‘AGRICULTURE AND LIVESTOCK)

PROGRAMU KATIKA KUNDI HILI NI KAMA ZIFUATAZO:-

 • ‘Leather Technology’;
 • ‘Food Technology and Human Nutrition’;
 • ‘Sugar Production Technology’;
 • ‘Veterinary Laboratory Technology’;
 • ‘Horticulture’;
 • ‘Irrigation Engineering’;‘Agro Mechanization’,
 • ‘Range Land Management and Tsetse fly control from Livestock”, and
 • ‘Sugarcane Production Technology’.

Mwongozo wa kuomba mkopo diploma, Mfano Wa Fomu Ya Mkopo HESLB PDF, Fomu Ya Kuomba Mkopo HESLB, Vigezo vya Kupata Mkopo ngazi ya diploma PDF Download, mwongozo wa utoaji mikopo 2023/2024, Mwongozo wa kuomba mkopo vyuo vya kati, Vigezo vya Kupata Mkopo HESLB dirisha la mkopo 2023/2024, Gpa ya kupata mkopo, Jinsi ya kuomba mkopo Online Mkopo kwa wanafunzi wa diploma, mwongozo wa kuomba mkopo 2023/24 pdf

7.0 VIPENGELE NA VIWANGO VYA MKOPO

Waombaji watakaopangiwa mikopo watapangiwa viwango vya fedha
kulingana na mahitaji halisi ya vyuoni.

Mkopo utagawanywa katika
vipengele vya mkopo kwa mtiririko ufuatao:

 • Chakula na Malazi,
 • Ada ya Mafunzo,
 • Gharama za Vitabu na viandikwa,
 • Mahitaji maalumu ya Kitivo,
 • Gharama za Utafiti na Mafunzo kwa Vitendo.

Mkopo utatolewa kwaajili ya kugharamia vipengele vyote au baadhi ya vipengele, kama itakavyochambuliwa na kuidhinishwa.

7.1 CHAKULA NA MALAZI

Kiwango cha juu kisichozidi TZS. 7,500.00 kwa siku kitatolewa
kulingana na idadi ya siku mwanafunzi atakuwa chuoni kama inavyoelekezwa kwenye kalenda ya chuo husika. Kiasi hiki kitalipwa moja kwa moja kwa mwanafunzi.

7.2 ADA YA MAFUNZO

Kiwango cha juu cha ada kisichozidi TZS. 1,400,000.00 kwa mwaka kulingana na gharama zinazolipwa katika chuo husika kwa mwaka na kitalipwa moja kwa moja kwa chuo husika.

7.3 GHARAMA ZA VITABU NA VIANDIKWA

Kiwango cha juu cha kisichozidi TZS. 200,000.00 kwa mwaka kwa
vitabu na viandikwa na kitatolewa kwa wanafunzi.

7.4 MAHITAJI MAALUMU YA KITIVO

Kiwango cha juu kisichozidi TZS. 300,000.00 kwa mwaka kulingana
na gharama husika zitalipwa moja kwa moja chuoni.

7.5 MAFUNZO KWA VITENDO
Kiwango cha juu kisichozidi TZS. 7,500.00 kwa siku hadi siku 56 kwa
mwaka, kwaajili ya Mafunzo kwa Vitendo kitatolewa.

Kiasi hicho kitalipwa moja kwa moja kwa mwanafunzi.

7.6 GHARAMA ZA KAZIMRADI

Kiasi kisichozidi TZS. 100,000.00 kwa mwaka kitatolewa kwa gharama za kazimradi kwa baadhi ya programu kama zilivyoainishwa na chuo husika.

8.0 MASHARTI MENGINE

8.1 WAJIBU WA MDHAMINI NA MZAZI/MLEZI

Wazazi/Walezi na wadhamini wana wajibu wa kuthibitisha usahihi wa taarifa ambazo zitawasilishwa katika fomu ya maombi ya mkopo kabla ya kusaini. Mdhamini/Mzazi atatakiwa kuhakikisha kwamba mkopaji anajaza taarifa sahihi zitakazotumika wakati wa urejeshaji.

Aidha mdhamini atatakiwa kutoa taarifa za mkopaji na makazi pale atakapochelewa au kushindwa kurejesha mkopo wake.

Kwa mwanafunzi alie na umri chini ya miaka 18 wakati wa kuomba mkopo atalazimika kujaza tamko rasmi (declaration) kuridhia kuendelea kupokea mkopo pindi atakapotimiza umri wa miaka 18.

Mwombaji wa mkopo anapaswa kuambatanisha picha (passport size) ya mdhamini na nakala ya kitambulisho kimojawapo kati ya vilivyotajwa hapo chini ambacho
kimetolewa na mamlaka za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania au Serikali ya Mapinduzi Zanzibar:-

 • Kitambulisho cha Taifa
 • Kadi ya mpiga kura
 • Leseni ya udereva
 • Pasi ya kusafiria
 • Kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi

8.2 UREJESHAJI MKOPO

Baada ya kuhitimu masomo ya elimu ya kati, mnufaika wa mkopo atatakiwa kurejesha mkopo wake wote kwa
makato yasiyopungua asilimia kumi na tano (15%) ya mshahara wake wa kila mwezi au kiwango kisichopungua TZS 100,000.00 kwa mwezi kwa Mnufaika aliyejiajiri kwenye sekta isiyo rasmi.

Iwapo mnufaika ataachishwa/atakatisha masomo, mkopo huo wote utalipwa kwa mkupuo. Mikopo yote inatozwa asilimia moja (1%) ya ada ya uendeshaji kwenye deni la msingi la mnufaika kwa mara moja.

9.0 KUHAMA CHUO AU
PROGRAMU NDANI YA CHUO

Endapo Mnufaika wa mkopo atabadilisha programu ya masomo ndani ya chuo chake, mkopo/stahili zake zitahamishwa na HESLB baada ya kupokea uthibitisho wa huo chake.

HESLB haitafanya malipo kwa wanafunzi ambao watahamia vyuo vingine kwa hiari yao amabkuhamia programu ambazo sio za kipaumbele zilizotajwa katika kipengele cha 6 cha mwongozo huu.

Uhamisho wa mkopo hautabadilisha kiwango cha mkopo kilichopangwa awali isipokuwa tu pale ambapo mwanafunzi
amehamishwa na mamlaka.

10.0 JINSI YA KUOMBA

Maombi yote ya mkopo yatafanyika kupitia Mfumo wa Maombi na Usimamizi wa Mikopo (OLAMS).

Waombaji wote wa mikopo WANAKUMBUSHWA kutumia namba ileile ya Mtihani wa Kidato cha Nne iliyotumika wakati wa udahili.

Baada ya kukamilika kwa mchakato wa maombi kwenye mtandao, waombaji watapaswa kupakua nakala za fomu
za maombi na mikataba ya mkopo kwenye mtandao, kugonga mihuri sehemu husika, kusaini fomu, kuambatanisha nyaraka zinazohitajika na kuziwasilisha kurasa zilizosainiwa (namba 2 na 5) ya fomu ya maombi katika OLAMS.

Mwombaji anatakiwa kupakua fomu sahihi kwa kuzingatia fomu ya mwombaji aliye na umri chini ya miaka 18 ama aliye juu ya miaka 18.

11.0 ADA YA MAOMBI YA MKOPO

Waombaji wanapaswa kulipia ada ya maombi ya mkopo ya kiasi cha shilingi elfu thelathini (30,000.00) kwa namba ya
kumbukumbu ya malipo wanayoipata katika mfumo na kulipia kupitia Benki (NMB, CRDB, TCB, NBC) au kwa mitandao
ya simu (Airtel Money, HaloPesa, T-Pesa, AzamPesa, M-Pesa, EzyPesa/TigoPesa).

Kwa maelezo zaidi tembelea:
https://olas.heslb.go.tz.

12.0 ORODHA YA WAOMBAJI WATAKAOPANGIWA MIKOPO

Orodha ya waombaji mikopo watakaopangiwa mikopo itatangazwa kupitia akaunti za kudumu za waombaji mikopo (SIPA) zilizotumiwa wakati wa kuomba mkopo au kwenye tovuti ya HESLB: www.heslb.go.tz baada ya mikopo kuidhinishwa.

13.0 MAULIZO NA MALALAMIKO

Waombaji au wanufaika wa mikopo wenye maswali au malalamiko watapaswa kufuata taratibu zilizoainishwa kwenye dawati la msaada la dirisha la maombi ya mkopo.

HESLB loan statement, HESLB news today, HESLB Login my account login password, HESLB Login continuous, Majina ya Waliopata Mkopo, HESLB allocation Status login, HESLB loan statement, HESLB news today, HESLB Login my account login password, HESLB Login continuous, Majina ya Waliopata Mkopo, HESLB allocation Status login.

PIA UNAWEZA KUSOMA👇

Tags: , , , , , , , , , ,

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Nijuze Habari WhatsAp Channel
  Nijuze Habari WhatsAp Group
  Nijuze Habari Telegram Channel