MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPA


RATIBA YA ROBO FAINALI CAF CHAMPIONS LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPARATIBA YA NUSU FAINALI CAF CHAMPIONS LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPA


RATIBA YA SIMBA ROBO FAINALI CAF CHAMPIONS LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPA


RATIBA YA YANGA ROBO FAINALI CAF CHAMPIONS LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPA


IJUE Saratani ya Tezi Dume

Filed in Makala, Michezo by on 27/02/2024 0 Comments

IJUE Saratani ya Tezi Dume

IJUE Saratani ya Tezi Dume, Dalili za tezi dume na tiba yake, Dawa YA TEZI DUME, Tiba asili ya tezi dume, Madhara ya upasuaji wa tezi dume, Tezi dume in English Vyakula vinavyozuia tezi dume.IJUE Saratani ya Tezi Dume, Dalili za tezi dume na tiba yake, Dawa YA TEZI DUME, Tiba asili ya tezi dume, Madhara ya upasuaji wa tezi dume, Tezi dume in English Vyakula vinavyozuia tezi dume.

SARATANI YA TEZI DUME

Tezi dume ni nini?

Tezi dume ni tezi inayopatikana kwa jinsia ya kiume. Tezi hii ina kazi ya kutengezeza  majimaji meupe mepesi yenye unato kidogo. Majimaji haya husaidia mbegu za kiume kutembea kwa urahisi.

Ipo wapi?

Tezi dume iko mwishoni mwa kibofu cha mkojo. Pia inauzunguka mrija unaounganisha kibofu cha mkojo na na mrija wa mkojo  wa uume (urethra) na iko mbele kidogo ya utumbo mpana ndani ya fupa la nyonga.

       Saratani ya tezi dume ni nini?

Saratani ya tezi dume maana yake ni tezi dume imepata ugonjwa wa saratani..Na hii hutokea pale ambapo chembechembe hai za tezi huasi na kuanza kujigawanya bila kufuata utaratibu wa mfumo wa mwili, chembechembe asi hizi mwishowe hutengeneza vivimbe hatari ndani ya tezi dume na hatimaye husambaa mwilini

Visababishi hatarishi kwa saratani ya Tezi dume

Umri  Mkubwa  kuanzia miaka 50

Nasaba (ukoo wenye historia a saratani hii

Lishe hatarishi-nyama nyekundu kwa wingi, mafuta/samli,maziwa ya krimu

Unene uliokithiri

Ukosefu wa mazoezi

Upungufu wa virutubisho,mfano vit D.

Maambukizi ya mara kwa mara kwenye tezi dume

      Dalili zake ni zipi?

 • Udhaifu katika utoaji wa mkojo, mkojo hauishi.
 • Kwenda kukojoa mara kwa mara.
 •  Damu ndani ya mkojo.
 • Kushindwa kukojoa.
 • Maumivu ya kiuno na mifupa ya nyonga.
 • Wagonjwa wengi huanza maumivu ya nyonga kama ni dalili za awali.
 • Udhaifu katika utoaji wa mkojo pia kunaweza kutokea kwa kuvimba kwa tezi dume bila ya saratani.
 • Damu kwenye mkojo nakushindwa kumaliza mkojo ni ishara tosha ya kuwa  tezi dume imeathirika.

UCHUNGUZI

Wanaume wote wanpaswa kufanya uchunguzi wa saratani ya tezi dume kuanzia miaka 50. Kwa wale wenye historia katika familia wanapaswa kuanza wakiwa na umri wa miaka 45.

Uchunguzi unafanyika kwa njia zifuatazo

 • Uchunguzi kwa cancer marker kwa kuchunguza damu (PSA).
 • Uchunguzi kwa njia ya kipimo cha njia ya haja kubwa (DRE)
 • Biopsy.
 • Ultrasound.
 • X-ray.
 • Bone scan.

      Jinsi ya kutibu saratani ya tezi dume

 • Upasuaji.
 • Mionzi
 • Dawa ya saratani
 • Homoni.

Matibabu hutegemea

 • Ngazi na ukali wa ugonjwa.
 • Je, ugonjwa upo ndani ya tezi dume tu au umesambaa.
 • Umri na afya ya mgonjwa.
 • Magonjwa ambatanishi na saratani hiyo, shinikizo la damu, matatizo ya moyo na kisukari.

       TIBA

      UPASUAJI

 • Kuondoa tezi dume yote peke yake inaweza ikatosha.
 • Kuondoa tezi dume na tezi jirani.
 • Kuondoa tezi dume na kuhasi
 • Kuondoa tezi dume kidogo kupitia njia ya mkojo na kumpa mgonjwa tiba shufa.

MIONZI.

 • Sawa na upasuaji inaweza kuondoa ugonjwa iwapo haujasambaa.
 • Mionzi pia hutolewa kama tiba shufaa.

DAWA YA SARATANI

Baadhi ya wagonjwa hufaidika na tiba hii, dawa hutolewa kwa muda mfupi na kufuatilia maendeleo ya mgomjwa kwa kufanya PSA,dawa inaweza kuwa moja au mchanganyiko.

HOMONI

Hutolewa mfullulizo kwa njia ya vidonge au sindano.

Ufuatiliaji wa karibu

Ni muhimu kufuatilia hali ya tezi isirejee baada ya ugonjwa kutibiwa kwa kufanya kipimo cha PSA mara kwa mara angalau miezi mitatu mara moja.

Athari zitokanazo na matibabu mbalimbali yaliyotajwa.

Upasuaji

Unaweza kusababisha kutoweza:

 • Kuzuia mkojo
 • Kupoteza nguvu za kiume.

Homoni

 • Homoni huongeza joto mwilini
 • Kupungukiwa na nguvu za kiume

Tiba ya tezi dume bila upasuaji, Tezi dume picha, Dawa ya tezi dume muhimbili, Maana ya tezi dume, Tezi dume na nguvu za kiume,Tezi dume ni busha.

PIA UNAWEZA KUSOMA👇

Tags: , , , , ,

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Nijuze Habari WhatsAp Channel
  Nijuze Habari WhatsAp Group
  Nijuze Habari Telegram Channel