MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPA


RATIBA YA ROBO FAINALI CAF CHAMPIONS LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPARATIBA YA NUSU FAINALI CAF CHAMPIONS LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPA


RATIBA YA SIMBA ROBO FAINALI CAF CHAMPIONS LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPA


RATIBA YA YANGA ROBO FAINALI CAF CHAMPIONS LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPA


KAGERA Veterans Mabingwa Muhalila Cup 2022/2023

Filed in Michezo by on 31/10/2023 0 Comments

KAGERA Veterans Mabingwa Muhalila Cup 2022/2023

VIDEO: Kagera Veterans Mabingwa Muhalila Cup 2022/2023

VIDEO: Kagera Veterans Mabingwa Muhalila Cup 2022/2023

KAGERA Veterans Mabingwa Muhalila Cup 2022/2023,Bukoba Veterans All Stars Mabingwa wapya Muhalila Cup 2022/2023, Bukoba Veteran FC Mabingwa wapya Muhalila Cup 2022/2023.

Mashindano ya Muhalila Cup msimu wa 2022/2023 yaliyofunguliwa tarehe 30 November, 2022 yalifikia tamati January mosi 2023 na Kagera Veterans FC ndio Mabingwa wa mashindano hayo baada kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Manyora FC kwenye mchezo wa Fainali.

Mamia ya wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa wa Kagera na Wilaya ya Muleba walijitokeza kwa wingi kushuhudia Fainali hiyo, ambapo Bukoba Veteran FC walitawazwa kuwa Mabingwa wapya wa msimu 2022/2023.

Bao moja lilitosha kuipa Ubingwa Bukoba Veterans All Stars au Kagera Veteran FC, likifungwa na kiungo Mshambuliaji Dickson dakika ya 22 baada ya kuwachambua walinzi wa Manyora FC na kupiga shuti kali lililomshinda mlinda lango wa Manyora na kujaa wavuni.

Kagera Veterans wanabeba Ubingwa huo ikiwa ni mara yao ya kwanza kushiriki Mashindano hayo tangu yaanzishwe mwaka 2015.

Mashindano hayo yalifanyika kwenye Viwanja vya Shule ya Sekondari ya Kagoma vilivyopo Kata ya Kagoma Wilaya ya Muleba Mkoa wa Kagera.

Mgeni rasmi kwenye Mashindano hayo alikuwa Bw.Tele Gama ambaye ni Mkurugenzi wa Kiwanda Cha Mali Juice kilichopo Wilayani Muleba.

VIDEO: Kagera Veterans Mabingwa Muhalila Cup 2022/2023

Muandaaji wa Mashindano hayo ambavyo yalishirikisha timu 16 zilizokuwa kwenye makundi manne ni Adv.Fotunatus Muhalila.

Timu zilizoshiriki Muhalila Cup msimu wa 2022/2023 zilikuwa ni;
1:Nsisha FC
2:Iroba FC
3:Bureza FC
4:Kakindo FC
5:Buhaya Stars
6: Muleba Heroes
7:Mchangani FC
8:Rwanganilo FC

9:Kagoma FC
10: Muleba Stars
11:Manyora FC
12:Ihumbo FC
13:Kikuku CC
14:Makarwe FC
15:Katoke FC na
16: Bukoba Veteran

Historia ya Ubingwa Muhalila Cup

2015/2016: Nsisha FC
2016/2017: Kikuku FC
2017/2018: Muyenje FC
2018/2019: Nsisha FC
2019/2020: Nsisha FC
2020/2021: Rubumba FC
2021/2022: Nsisha FC
2022/2023: Bukoba Veterans FC

VIDEO: TAZAMA JINSI VETERANS FC WALIVYOCHUKUA KOMBE MUHALILA CUP MSIMU WA 2022/2023

KAGERA Veterans Mabingwa wapya Muhalila Cup 2022/2023

KAGERA Veterans Mabingwa wapya Muhalila Cup 2022/2023

Kocha Mkuu wa Manyora Fc akisalimiana na Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Mali Juice Muleba Bw.Tele Gama na kukabidhiwa zawadi za mshindi wa Pili.

Kocha Mkuu wa Manyora Fc akisalimiana na Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Mali Juice Muleba Bw.Tele Gama na kukabidhiwa zawadi za mshindi wa Pili.

Zawadi ya Mchezaji bora MZAWA wa Mashindano imechukuliwa na YARID HAMDANI mchezaji wa Nsisha Fc.

Zawadi ya Mchezaji bora MZAWA wa Mashindano imechukuliwa na YARID HAMDANI mchezaji wa Nsisha Fc.

 

Kipa Bora ni wa Kagera Veteran Fc akipokea zawadi yake kutoka kwa Adv.Fortunatus Muhalila.

Kipa Bora ni wa Kagera Veteran Fc akipokea zawadi yake kutoka kwa Adv.Fortunatus Muhalila.

Mchezaji wa Kagera Veterans Fc "Abbas" akipokea zawadi ya Mfungaji bora kutoka kwa Mgeni rasmi.

Mchezaji wa Kagera Veterans Fc “Abbas” akipokea zawadi ya Mfungaji bora kutoka kwa Mgeni rasmi.

Mwalimu Godwin Adolf Kahinga "Nyonge" akipokea zawadi kwa kusimamia vema ligi ya MuhalilaCup2022 kama mratibu mkuu.

Mwalimu Godwin Adolf Kahinga “Nyonge” akipokea zawadi kwa kusimamia vema ligi ya MuhalilaCup2022 kama mratibu mkuu.

Zawadi ya Mshindi wa Tatu imekwenda Kikuku Fc.

Zawadi ya Mshindi wa Tatu imekwenda Kikuku Fc.

PIA UNAWEZA KUSOMA👇

Tags: , , ,

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Nijuze Habari WhatsAp Channel
  Nijuze Habari WhatsAp Group
  Nijuze Habari Telegram Channel