MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPA


RATIBA YA ROBO FAINALI CAF CHAMPIONS LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPARATIBA YA NUSU FAINALI CAF CHAMPIONS LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPA


RATIBA YA SIMBA ROBO FAINALI CAF CHAMPIONS LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPA


RATIBA YA YANGA ROBO FAINALI CAF CHAMPIONS LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPA


Kocha Mpya Simba SC Atajwa

Filed in Michezo by on 01/11/2021 0 Comments

Soma: Matokeo ya Darasa la Saba 2021

Soma: Wanafunzi waliofutiwa Matokeo ya Darasa la Saba 2021

Soma: Wanafunzi 10 Bora Matokeo ya Darasa la Saba 2021

Soma: Shule 10 Bora Matokeo ya Darasa la Saba 2021

Soma: Magazeti ya Jumatatu November 01,2021

Soma: Kikosi Cha Tanzania Kufuzu Kombe la Dunia vs DR Congo & Madagascar

MTENDAJI Mkuu wa Klabu Bingwa Tanzania Bara Simba SC, Barbara Gonzalez amesema malengo ya Klabu hiyo kwa sasa, ni kumuajiri kocha kutoka Barani Afrika kwaajili ya kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Kocha Didier Gomes ambaye aliondoka Klabuni hapo.

Inaelezwa kuwa Uongozi wa Klabu ya Simba SC, umeshaanza mzungumzo na Kocha Msaidizi wa Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, Rulani Mokwena kuwa Kocha Mkuu wa kikosi hicho chenye makazi yake mtaa wa Msimbazi Jijini Dar es salaam.

Barbara amesema Uongozi wa Simba SC unaendelea kufanya mchakato wa kumpata kocha bora atakayekinoa kikosi chao, baada ya kuondoka kwa Gomes, hivyo wanachama na mashabiki wanapaswa kuwa wavumilivu katika kipindi hiki.

“Suala la kocha halihitaji kukurupuka, kwani tunaweza kumpata mwenye wasifu mkubwa lakini akashindwa kutibu matatizo yaliyopo katika kikosi cha Simba na shida ikabaki pale pale,”

“Kama atakuwa Mokwena au mwingine hilo litajulikana ndani ya muda mfupi, lakini malengo ya klabu ni kumpata kocha kutoka Afrika na si Mzungu kama aliyetoka”

“Tunaweza kumpata kocha wa Afrika ambaye tunamuhitaji na wasifu wake usiwe mkubwa na akaweza kuisaidia timu kufikia malengo yake kwani atakuwa na kiu ya mafanikio na tutadumu naye kwa muda mrefu”

“Angalia klabu kama Chelsea wakati wanamchukua Thomas Tuchel wengi hawakuwa na imani naye, ila baada ya muda mfupi ameifanya timu kucheza vizuri na kushinda ubingwa wa Ulaya.” Amesema Barbara.

Simba SC imeripotiwa kupokea maombi ya makocha zaidi ya 70, siku chache baada ya kuachana na Kocha Didier Gomes kufuatia kushindwa kufikia lengo la kutinga hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika 2021/2022 la Klabu hiyo.

Tags: , ,

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Nijuze Habari WhatsAp Channel
  Nijuze Habari WhatsAp Group
  Nijuze Habari Telegram Channel