MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPA


RATIBA YA ROBO FAINALI CAF CHAMPIONS LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPARATIBA YA NUSU FAINALI CAF CHAMPIONS LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPA


RATIBA YA SIMBA ROBO FAINALI CAF CHAMPIONS LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPA


RATIBA YA YANGA ROBO FAINALI CAF CHAMPIONS LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPA


MASWALI na Majibu Katika Utumishi Portal

Filed in Ajira, Michezo by on 11/02/2024 0 Comments

MASWALI na Majibu Katika Utumishi Portal

MASWALI na Majibu Katika Utumishi Portal, Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara,Maswali na Majibu Kwa Watumiaji wa Huduma Katika Watumishi Portal, Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara Ajiraportal.

MASWALI na Majibu Katika Utumishi Portal

MASWALI na Majibu Katika Utumishi Portal, Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara,Maswali na Majibu Kwa Watumiaji wa Huduma Katika Watumishi Portal, Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara Ajiraportal.

A. Maswali yanayoulizwa mara kwa mara kuhusiana na Usajili, Kusahau Nywila na Ku-reset Password.

1.Najaribu kujisajili ninaletewa ujumbe “The email address you are trying to register with is not the same as in your HCMIS profile.”

 • Hii inasababishwa na email unayotumia kujisajili haifanani na email iliyopo kwenye taarifa zako kwenye Mfumo wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara Serikalini (HCMIS).
 • Kutatua changamoto hii unapaswa kuwasiliana na Afisa Utumishi wako ili ahuishe taaifa zako ikiwepo kukuwekea email unayotaka kujisajili nayo pamoja na namba ya simu ya mkononi unayotumia kwenye Mfumo wa HCMIS.
 • Pia Mtumishi anapewa angalizo kuhakikisha barua pepe (email) anayotumia kujisajili ni ya kwake na anaweza kuifungua na kusoma emails.
 • Hii ni muhimu kwa sababu pindi anapojisajili nywila (Password) hutumwa kwenye barua pepe hii.

2.Nimekosea barua pepe, barau pepe ya mwanzo niliotumia kujisajili siitumii tena, Barua pepe niliyotumia kujisajili nimesahau nywila yake na nimeshindwa kuirejesha.

 • Iwapo utakuwa na changamoto yoyote kati ya hizo hapo juu utapswa kuwasiliana na Afisa Utumishi wako ili aweze kuhuisha taarifa zako wenye Mfumo wa HCMIS kwa kuweka barua pepe mpya unayotumia sasa.
 • Kisha utaenda kwenye Mfumo wa Watumishi Portal na kuomba kubadili nywila (Password Reset).
 • Utatumiwa Nywila Mpya kwenye barua pepe yako mpya.

3.Nikiweka au kubadilisha nywila (Password) naambiwa “weak password”

 • WAFUNGAJI Bora NBC Premier League 2023/2024
 • Password inatakiwa kuwa na mchanganyiko wa herufi kubwa [A-Z], herudi ndogo [a-z], namba [0-9] na alama maalum [!@#.]
 • na idadi isipungue herufi nane (8).
 • Mfano Maji@2025.
 • Aidha, Mtumishi aepuke kutumia taarifa kama tarehe za kuzaliwa, Majina ya kwake na wanafamilia wake na ndugu au jamaa za karibu.

4.Nikijisajili kwenye mfumo naambiwa “User already Exit by check number”

 • Hii inaashiria check number husika imeshatumika kufanya usajili.
 • Unapaswa kubofya kiunganishi cha “Forgot Password” kisha jaza taarifa (check Number na Email yako uliyotumia kujisajili) ili upatiwe nywila mpya.
 • Ukishindwa wasiliana na Afisa TEHAMA wa taasisi yako.

5.Nikijisajili kwenye mfumo naambiwa “User already Exit by email”

 • Hii inaashiria barua pepe (email) husika imeshatumika kufanya usajili.
 • Unapaswa kubofya kiunganishi cha “Forgot Password” kisha jaza taarifa (check Number na email yako uliyotumia kujisajili) ili upatiwe nywila mpya.
 • Ukishindwa wasiliana na Afisa TEHAMA wa taasisi yako.

6.Nikijisajili kwenye mfumo naambiwa “User already Exit by National Id”

 • Hii inaashiria namba ya NIDA (NIN) husika imeshatumika kufanya usajili.
 • Unapaswa kubofya kiunganishi cha “Forgot Password” kisha jaza taarifa (Check Number na Email yako uliyotumia kujisajili) ili upatiwe nywila mpya.
 • Ukishindwa wasiliana na Afisa TEHAMA wa taasisi yako.

7.Mfumo unaniambia “Wrong Credentials”

 • Mtumishi anapopata ujumbe wa aina hii maana yake “username” au “password” aliyoweka sio sahihi.
 • Mtumishi anapaswa kuweka taarifa zake kwa usahihi,
 • na kama amesahau nywila yake anaweza kubofya kiunganishi cha “Forgot Password” kisha jaza taarifa (Check Number na email yako uliyotumia kujisajili) ili upatiwe nywila mpya.

8.Nimejisajili lakini sijapokea ujumbe kwenye barua pepe yangu.

 • Ingia kwenye barua pepe yako sehemu ya “INBOX” kama ujumbe haupo nenda kwenye sehemu ya “SPAM” au “BLOCKED MAILS” kama sehemu zote hakuna ujumbe unaweza kubofya kiunganishi cha “Forgot Password” kisha jaza taarifa (Check Number na email yako uliyotumia kujisajili) ili upatiwe nywila mpya.
MASWALI na Majibu Katika Utumishi Portal, Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara,Maswali na Majibu Kwa Watumiaji wa Huduma Katika Watumishi Portal, Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara Ajiraportal.

MASWALI na Majibu Katika Utumishi Portal

B. Maswali na majibu kwenye huduma ya Uhamisho (e-Transfer)

1.”Supervisor” wangu haoni ombi nililomtumia

 • Ili msimamizi aweze kuona maombi ya watumishi walioko chini yake atapaswa awe amejisajili.
 • Pia Afisa TEHAMA wa Taasisi husika atatakiwa kumpatia “Supervisor role” kulingana na majukumu yake mfano mkuu wa sehemu, kituo cha kazi, idara au kitengo.
 • Kuthibitisha hili wasiliana na Afisa TEHAMA wa taasisi yako.
 • Maombi ya uhamisho yanaonekana baada ya supervisor kubofya “Transfer Requests” upande wa kushoto.
 • Kama ni mkuu wa sehemu au kituo cha kazi ataona maombi ndani ya menu imeandikwa “Workstation Supervior Transfer Approval”.
 • Kama ni mkuu wa Idara au kitengo ataona maombi ndani ya menu imeandikwa “Department/Unit Transfer Approval”
 • Kama ni mkuu wa sehemu ataona maombi ndani ya menu imeandikwa “Section Supervisor Transfer Approval”

2.Mfumo unanipa ujumbe “No teaching Subject”

 • Mtumishi ambaye ni mwalimu wa Sekondari anapaswa kuwa na masomo ya kufundishia kwenye Mfumo wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara (HCMIS).
 • Iwapo taarifa hizi hazijawekwa mtumishi atapata ujumbe huu wa “No teaching Subject” pindi atakapotaka kuomba uhamisho.
 • Kutatua changamoto hii mtumishi atatakiwa kuwasiliana na Afisa Utumishi aweze kukuwekea masomo unayofundisha

3.Naambiwa nina “pending request” nikiwa nataka kuomba uhamisho wa kubadilishana.

 • Mtumishi anaweza kuomba kuhama, au kubadilishana kituo mara moja tu kwa kipindi kimoja.
 • Iwapo utakuwa na maombi yanasubiri Idhini, au una maombi ya kubadilishana kituo ambayo bado haujapata mtu wa kubadilishana naye na ukajaribu kunzisha maombi mengine bila kufuta ya awali mfumo utakuletea ujumbe huu wa “pending request”.
 • Unatakiwa kuwa na ombi moja kwa wakati, kwahiyo mtumishi anatakiwa kufuta ombi lake alilotengeneza kabla kusajili ombi lingine.

C.Maswali na majibu kwenye huduma ya Taarifa Binafsi (My Profile)

1.Taarifa zangu (mfano Cheo, Idara, Sehemu, Kituo cha Kazi, Tarehe za Kuajiriwa au Kuthibitishwa kazini, Baruapepe, Namba za Simu, n.k) sio sahihi.

 • Mtumishi atakayeona kwenye profile yake taarifa zake haziko sahihi, anapaswa kuwasiliana na Afisa Utumishi wake akiwa na vithibitisho vya taarifa zake sahihi.
 • Afisa Utumishi baada ya kujiridhisha atatakiwa kufuata taratibu zote zinazopaswa kuhakikisha anahuisha taarifa za mtumishi kwenye Mfumo wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara.

2.Taarifa zangu (mfano Cheo, Idara, Sehemu, Kituo cha Kazi, Tarehe za Kuajiriwa au Kuthibitishwa kazini, Baruapepe, Namba za Simu, n.k) hazipo.

 • Mtumishi atakayeona kwenye profile yake taarifa zake haziko sahihi, anapaswa kuwasiliana na Afisa Utumishi wake akiwa na vithibitisho vya taarifa zake sahihi.
 • Afisa Utumishi baada ya kujiridhisha atatakiwa kufuata taratibu zote zinazopaswa kuhakikisha anahuisha taarifa za mtumishi kwenye Mfumo wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara.

D.Maswali na majibu kwenye huduma ya e-Mkopo (e-Loan)

1.Nikitaka kuomba mkopo naambiwa “No phone number or phone number is invalid please contact your employer”

 • Mtumishi anayekutana na changamoto hii anapaswa kuingia kwenye profile yake kuhakiki taarifa ya namba yake ya simu.
 • Kama namba yake ya simu haiko sawa, ni namba aliyokuwa akitumia zamani na sasa haitumii, kama imeandikwa vibaya au namba ya simu hakuna kabisa kwenye profile yake awasiliane na Afisa Utumishi wake ili arekebishe taarifa husika.

2.Sijapata msimbo wa kuthibitisha ombi la mkopo (OTP) kwenye simu yangu wakati wa kutuma ombi la mkopo.

 • Hakikisha namba iliopo kwenye profile yako ni sawa na unayotegemea kupata ujumbe husika.
 • Kama ni tofauti wasiliana na Afisa Utumishi wako ili aweze kuhuisha taarifa zako (namba ya simu).
 • Aidha kama namba ni sahihi, jaribu mara nyingine tena kwani inaweza kuwa changamoto ya mtandao.
 • Iwapo utajaribu zaidi ya mara tatu na haupati msimbo tafadhali wasiliana na huduma kwa kutuma barua pepe kwenda [email protected] au Simu 026 2160240.
 • Pia iwapo ulianzisha ombi la mkopo kisha ukabadili namba ya simu kwenye mfumo, tafadhali futa ombi hilo ili uanzishe ombi upya.

3.Mfumo unaniambia “invalid account number” wakati wakuhifadhi ombi la mkopo.

 • Hakikisha unaweka akaunt namba sahihi kama inavyosomeka kwenye taarifa za Benki husika.
 • Hauwezi kutumia Akaunti namba ya Benki nyingine kuombea Mkopo kwenye Benki nyingine

4.Mfumo unaniambia “Dormant account number” wakati wakuhifadhi ombi la mkopo Ili uweze kukopa,

 • Akaunti ya benki unayotarajia kupokea fedha za mkopo inapaswa kuwa hai.
 • Ikiwa haujatumia akaunti hiyo kwa zaidi ya miezi sita(6) tafadhali wasiliana na Benki husika ili kuhuisha akaunti yako kabla ya kuomba mkopo.

5.Mfumo unaniambia “Names missmatch” wakati wakuhifadhi ombi la mkopo.

 • Hakikisha majina yako kwenye taarifa za Ajira (kwenye Profile yako na Mfumo wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara – HCMIS) ni sawa sawa na majina yaliopo kwenye taarifa za akaunt ya Benki husika

Maswali ya afisa utumishi, Mshahara wa afisa utumishi ngazi ya degree, Majukumu ya afisa utumishi, Sifa za kuwa afisa utumishi, Afisa utumishi ni nani, Afisa utumishi in english, Kanuni za utumishi wa umma za mwaka 2024 pdf, Madaraja ya utumishi 2024, Sheria ya utumishi wa umma 2024 pdf, Majukumu ya afisa rasilimali watu, Muundo mpya wa utumishi wa umma 2024, Utumishi wa umma ni nini.

PIA UNAWEZA KUSOMA👇

Tags: , , ,

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Nijuze Habari WhatsAp Channel
  Nijuze Habari WhatsAp Group
  Nijuze Habari Telegram Channel