MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPA


RATIBA YA ROBO FAINALI CAF CHAMPIONS LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPARATIBA YA NUSU FAINALI CAF CHAMPIONS LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPA


RATIBA YA SIMBA ROBO FAINALI CAF CHAMPIONS LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPA


RATIBA YA YANGA ROBO FAINALI CAF CHAMPIONS LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPA


Matokeo KMC FC vs Young Africans SC

Filed in Michezo by on 19/10/2021 0 Comments

KLABU ya Young Africans SC imeendeleza wimbi la ushindi kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara (NBC Premier League) baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji KMC FC jioni ya leo kwenye Uwanja wa MajiMaji mjini Songea mkoani Ruvuma.

Nyota wa mchezo huo ni kiungo wa kimataifa wa Tanzania, Feisal Salum Abdallah aliyefunga bao la Pili na kutoa pasi ya bao la kwanza mapema kipindi cha kwanza na kuifanya timu hiyo iliyo chini ya kocha Mtunisia, Nasreddine Nabi anayesaidiwa kazi na Mrundi, Cedric Kaze ifikishe pointi tisa (9) baada ya kucheza mechi tatu za awali, mbili ikicheza ugenini.

Fiston Mayele aliifungia Young Africans bao kwanza baada ya shuti kali la Feisal Salum Abdallah lililombabatiza mshambuliaji huyo raia DR Congo na kuingia kimiani kwenye dakika ya 5.

Feisal Salum Abdallah akaifungua Young Africans SC bao la pili na la ushindi kwenye dakika ya 10 kwa shuti kali pia lenye umbali wa mita 25 baada ya kutengewa pasi na Fiston Kalala Mayele.

Tags: , , , ,

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Nijuze Habari WhatsAp Channel
  Nijuze Habari WhatsAp Group
  Nijuze Habari Telegram Channel