MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPA


RATIBA YA ROBO FAINALI CAF CHAMPIONS LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPARATIBA YA NUSU FAINALI CAF CHAMPIONS LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPA


RATIBA YA SIMBA ROBO FAINALI CAF CHAMPIONS LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPA


RATIBA YA YANGA ROBO FAINALI CAF CHAMPIONS LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPA


Matokeo Simba SC vs Polisi Tanzania FC

Filed in Michezo by on 28/10/2021 0 Comments

MABINGWA watetezi Simba SC, wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Polisi Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara ulichezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Ushindi huo haukuwa ushindi mwepesi, kwani wenyeji hao walilazimika kusubiri hadi dakika ya 89 kuweza kupata bao hilo pekee tena kwa mkwaju wa penalti kutoka kwa kiungo Mzambia, Rally Bwalya.

Baada ya ushindi huo Simba SC inafikisha pointi saba (7) baada ya kucheza mechi tatu, kufuatia kutoa sare mechi ya kwanza vs Biashara United Mjini Musoma mkaoni Mara kabla ya kushinda 1-0 vs Dodom Jiji FC Jijini Dodoma.

Huo unakuwa mchezo wa kwanza kupoteza kwa Polisi Tanzania ya Moshi mkoani Kilimanjaro baada ya mwanzo mzuri wakifanikiwa kushinda mechi tatu mfululizo

Hivi ndivyo mambo yalivyo kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League) baada ya mechi mbili zilizochezwa jana Jumatano October 27, 2021, ukionesha Polisi Tanzania FC ikishuka kwa nafasi moja wakati Simba ikipanda kwa nafasi sita.

Tags: , , , ,

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Nijuze Habari WhatsAp Channel
  Nijuze Habari WhatsAp Group
  Nijuze Habari Telegram Channel