MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPA


RATIBA YA ROBO FAINALI CAF CHAMPIONS LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPARATIBA YA NUSU FAINALI CAF CHAMPIONS LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPA


RATIBA YA SIMBA ROBO FAINALI CAF CHAMPIONS LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPA


RATIBA YA YANGA ROBO FAINALI CAF CHAMPIONS LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPA


Matokeo Yanga SC vs Ruvu Shooting November 02,2021

Filed in Michezo by on 02/11/2021 0 Comments

Soma: Matokeo ya Darasa la Saba 2021

Soma: Wanafunzi waliofutiwa Matokeo ya Darasa la Saba 2021

Soma: Wanafunzi 10 Bora Matokeo ya Darasa la Saba 2021

Soma: Shule 10 Bora Matokeo ya Darasa la Saba 2021

Soma: Magazeti ya Jumatatu November 01,2021

Soma: Kikosi Cha Tanzania Kufuzu Kombe la Dunia vs DR Congo & Madagascar

Soma: Kocha Mpya Simba SC Atajwa

Soma: Magazeti ya Jumanne November 02,2021

KLABU ya Young Africans SC imeendelea kujichimbia kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League) baada ya kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Ruvu Shooting FC.

Ruvu Shooting FC ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao kwenye dakika ya 9 kupitia kwa Shabani Msala ambaye shuti lake lilimgonga beki Kibwana Shomari na kumpoteza kipa wa Young Africans SC Djigui Diarra.

Feisal Salum ‘Fei Toto’ akairudisha Young Africans mchezoni dakika ya 33 baada ya kupiga shuti kali nje ya 18, likiwa ni bao lake la tatu msimu huu wa 2021/2022.

Young Africans ilirejea kipindi cha pili kusaka mabao zaidi na walifanikiwa kufunga bao la pili kwenye dakika ya 48 baada ya Ali Mtoni ‘Sonso’ kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari na mwamuzi Emmanuel Mwandembwa kuamuru mkwaju wa penati ambao uliwekwa kambani na Djuma Shabani.

Kiungo Mkongomani Mukoko Tonombe akaifungia Young Africans bao la 3 kwenye dakika ya 74 akiunganisha krosi ya winga Mtanzania Farid Mussa Marick.

Huo unakuwa ushindi wa tano (5) mfululizo kwa Young Africans kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League)

Tags: , , , ,

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Nijuze Habari WhatsAp Channel
  Nijuze Habari WhatsAp Group
  Nijuze Habari Telegram Channel