MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPA


RATIBA YA ROBO FAINALI CAF CHAMPIONS LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPARATIBA YA NUSU FAINALI CAF CHAMPIONS LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPA


RATIBA YA SIMBA ROBO FAINALI CAF CHAMPIONS LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPA


RATIBA YA YANGA ROBO FAINALI CAF CHAMPIONS LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPA


Matokeo Yanga vs Mbeya Kwanza

Filed in Uncategorized by on 01/12/2021 0 Comments

VINARA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Klabu ya Young Africans SC imetanua uongozi wao hadi pointi tano dhidi ya mabingwa watetezi, Simba SC baada ya kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji, Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.

Mabao ya Yanga SC yamefungwa na kiungo Mrundi, Said Ntibanzokiza kwa shuti la mpira wa adhabu dakika ya 18 na mshambuliaji Mkongo, Fiston Kalala Mayele dakika ya 26 akimalizia pasi ya kiungo Mzanzibar, Feisal Salum Abdallah ‘Fei Toto’.

Baada ya ushindi huo Young Africans SC inafikisha jumla ya pointi 19 baada ya mechi saba na kuendelea kuongoza Ligi kwa pointi tano zaidi ya watani wao wa jadi, Simba SC ambao wana mechi moja mkononi na dhidi ya Geita Gold kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Klabu ya Mbeya Kwanza baada ya kichapo hicho wanabaki na pointi zao saba baada ya kucheza mechi saba wakiwa kwenye nafasi ya 11.

Mechi nyingine za Ligi Kuu, Biashara United wamelazimishwa sare ya bao 1-1 na Polisi Tanzania kwenye Uwanja wa Karume mjini Musoma mkoani Mara.

Mshambuliaji Adam Adam aliwatanguliza wageni, Polisi dakika ya 46, kabla ya Nassib Mpapi dakika ya 61 kusawazisha bao hilo.

Biashara United inafikisha pointi nane na kusogea hadi nafasi ya saba, wakati Polisi Tanzania inafikisha pointi 11, ingawa inabaki kwenye nafasi ya tano baada ya timu zote kucheza mechi saba.

Bao pekee la mshambuliaji Mkongo, Idris Mbombo dakika ya 52 limetosha kuipa Azam FC ushindi wa 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu Tanzania Bara, mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi 10 na kusogea nafasi ya sita, wakati Mtibwa Sugar inabaki na pointi zake mbili baada ya timu zote kucheza mechi saba na kuendelea kushika mkia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Nijuze Habari WhatsAp Channel
  Nijuze Habari WhatsAp Group
  Nijuze Habari Telegram Channel