MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPA


RATIBA YA ROBO FAINALI CAF CHAMPIONS LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPARATIBA YA NUSU FAINALI CAF CHAMPIONS LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPA


RATIBA YA SIMBA ROBO FAINALI CAF CHAMPIONS LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPA


RATIBA YA YANGA ROBO FAINALI CAF CHAMPIONS LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPA


RAIS Samia Afanya Mabadiliko Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala na Wakuu wa Wilaya

Filed in Habari by on 09/03/2024 0 Comments

RAIS Samia Afanya Mabadiliko Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala na Wakuu wa Wilaya 

RAIS Samia Afanya Mabadiliko Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala na Wakuu wa Wilaya

RAIS Samia Afanya Mabadiliko Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala na Wakuu wa Wilaya

RAIS Samia Afanya Mabadiliko Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala na Wakuu wa Wilaya, Rais Dkt.Samia afanya mabadiliko madogo ya wakuu wa mikoa, makatibu tawala wa mikoa,wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko ya baadhi ya viongozi ambapo aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Abbas amehamishwa kutoka mkoa huo na kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi, Dkt. Moses Mpogole Kusiluka ambapo imeeleza kuwa, Rais Dkt. Samia pia amemhamisha Halima Omar Dendego kutoka Mkoa wa Iringa kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida.

Aidha, Peter Joseph Serukamba amehamishwa kutoka Mkoa wa Singida kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa.

Wakati huo huo, Balozi Batilda Salha Burian amehamishwa kutoka Mkoa wa Tabora kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga.

Vile vile Rais Dkt.Samia amemteua Daniel Chongolo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe.

Chongolo aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambapo miezi kadhaa iliyopita alijiuzulu nafasi hiyo.

Taarifa hiyo pia imeeleza kuwa Rais Dkt.Samia amemteua Patric Kenan Sawala kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Sawala alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba.

Naye Paul Matiko Chacha ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, awali alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Misungwi;

Utezi zaidi wa Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala, Wakuu wa Wilaya  na wakurugenzi wa halmashauri tazama hapa chini;

PIA UNAWEZA KUSOMA👇

Tags: ,

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Nijuze Habari WhatsAp Channel
  Nijuze Habari WhatsAp Group
  Nijuze Habari Telegram Channel