MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPA


RATIBA YA ROBO FAINALI CAF CHAMPIONS LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPARATIBA YA NUSU FAINALI CAF CHAMPIONS LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPA


RATIBA YA SIMBA ROBO FAINALI CAF CHAMPIONS LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPA


RATIBA YA YANGA ROBO FAINALI CAF CHAMPIONS LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPA


Ratiba ya Ligi Kuu mzunguko wa kwanza

Filed in Michezo by on 26/09/2021 0 Comments

PAZIA la Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa msimu wa 2021/2022 linatarajiwa kufunguliwa rasmi kesho Jumatatu ya September 27,2021.

Ufunguzi wa msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) 2021/2021 ulitanguliwa na mchezo wa Ngao ya Jamii uliopigwa jana Jumapili September 25 na Yanga kuibuka washindi mbele ya Mabingwa watetezi Simba SC.

Bao pekee lililoipa Yanga Ubingwa lilifungwa na Mshambuliaji mpya wa Klabu hiyo Fiston Kalala Mayele raia wa DR Congo kwenye dakika ya 11.

Kesho Jumatatu September 27,2021 itachezwa michezo mitatu tu, ambapo Mtibwa Sugar FC itawakaribisha Mbeya Kwanza kutoka Mbeya, saa 8:00 mchana kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Namungo FC ya Lindi itaikaribisha Geita Gold FC ya Geita saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Ilulu, Lindi.

Mchezo mwingine kesho Jumatatu utakuwa Kati ya Coastal Union FC ya Mara dhidi ya Azam FC saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Jumanne September 28,2021 itachezwa michezo mwingine mitatu, ambapo Dodoma Jiji FC wataikaribisha Ruvu Shooting FC saa 8:00 mchana kwenye Uwanja wa Jamhuri, Jijini Dodoma.

Mbeya City FC wao watawakaribisha majirani zao wajerajera Tanzania Prisons FC saa 10:00 jioni kwenye Uwanja Kumbukumbu ya Sokoine, Jijini Mbeya.

Mchezo mwingine wa Jumanne utakuwa kati ya wenyeji Biashara United FC ya Mara dhidi ya Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Simba SC saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa CCM Karume, Mara.

Jumatano September 29,2021 itachezwa michezo miwili kukamilisha mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu, ambapo Klabu ya Polisi Tanzania FC itaikaribisha KMC FC kwenye Uwanja wa Ushirika, Kilimanjaro saa 8:00 mchana.

Mchezo wa mwisho wa mzunguko wa kwanza utakuwa kati ya Kagera Sugar FC dhidi ya Young Africans SC saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Kaitaba Bukoba, Kagera.

Tags: , , , ,

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Nijuze Habari WhatsAp Channel
  Nijuze Habari WhatsAp Group
  Nijuze Habari Telegram Channel