MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPA


RATIBA YA ROBO FAINALI CAF CHAMPIONS LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPARATIBA YA NUSU FAINALI CAF CHAMPIONS LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPA


RATIBA YA SIMBA ROBO FAINALI CAF CHAMPIONS LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPA


RATIBA YA YANGA ROBO FAINALI CAF CHAMPIONS LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPA


Ratiba ya Raundi ya Pili Ligi Kuu Tanzania Bara

Filed in Michezo by on 29/09/2021 0 Comments

RATIBA ya raundi ya pili ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) 2021/2022, ambayo itapigwa kuanzia Ijumaa ya October 01, Jumamosi ya October 02 na Jumapili ya October 03,2021 kama ifuatavyo:-

Ijumaa ya October 01,2021 itapigwa Michezo miwili, Kati ya Dodoma Jiji FC vs Simba SC kwenye Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma kuanzia saa 10:00 jioni.

Mchezo mwingine utakuwa Kati ya Biashara United FC vs Ruvu Shooting FC kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume Mkoani Mara saa 10:00 jioni.

Jumamosi ya October 02,2021, itapigwa Michezo mitatu ambapo ni Kati ya Coastal Union FC vs KMC saa 8:00 mchana kwenye Uwanja wa Mkwakwani Tanga.

Mchezo mwingine Jumamosi utakuwa Kati ya Polisi Tanzania FC vs Azam FC saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Ushirika Moshi, Kilimanjaro.

Mchezo wa mwisho kwa Jumamosi utakuwa Kati ya Young Africans SC vs Geita Gold FC saa 1:00 usiku kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam.

Jumapili ya October 03, 2021, itapigwa Michezo mitatu katika kukamilisha raundi ya pili ya Tanzania Premier League msimu wa 2021/2022, ambapo mchezo wa kwanza itakuwa Kati ya Mtibwa Sugar FC vs Tanzania Prisons FC saa 8:00 mchana kwenye Uwanja Jamhuri, Morogoro.

Mchezo wa pili Jumapili itakuwa Derby ya Mbeya ambapo Mbeya City FC watawakaribisha Mbeya Kwanza FC saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine Jijini Mbeya.

Mchezo wa mwisho wa kufunga raundi ya pili ya Tanzania Premier League Jumapili ya October 3 utakuwa Kati ya Namungo FC vs Kagera Sugar FC saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Ilulu Lindi.

Tags: , , , , , ,

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Nijuze Habari WhatsAp Channel
  Nijuze Habari WhatsAp Group
  Nijuze Habari Telegram Channel