MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPA


RATIBA YA ROBO FAINALI CAF CHAMPIONS LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPARATIBA YA NUSU FAINALI CAF CHAMPIONS LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPA


RATIBA YA SIMBA ROBO FAINALI CAF CHAMPIONS LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPA


RATIBA YA YANGA ROBO FAINALI CAF CHAMPIONS LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPA


Simba yamtambulisha Kocha Mpya

Filed in Michezo, Usajili by on 06/11/2021 0 Comments

KLABUya Simba imemtangaza kocha Pablo Franco Martín raia wa Hispania mwenye umri wa miaka 41 kuwa Kocha mkuu wa klabu hiyo yenye makazi yake mtaa wa Msimbazi Jijini Dar es salaam akichukua nafasi ya Didier Gomes raia wa Ufaransa.

Soma: Matokeo ya Darasa la Saba 2021

Pablo anachukua nafasi hiyo baada ya mkataba wa Gomes kusitishwa hivi karibuni baada ya klabu hiyo kushindwa kufuzu hatua ya makundi ya klabu Bingwa Barani Afrika CAF Champion League.

Soma: Kikosi Cha Tanzania Kufuzu Kombe la Dunia vs DR Congo & Madagascar

Pablo aliyezaliwa Juni 11 mwaka 1980 ni kocha mwenye uzoefu aliyefundisha klabu mbalimbali nchini kwao, ikiwemo mabingwa wa kihistoria wa Ulaya Klabu ya Real Madrid.

Pablo mwenye umri wa miaka 41, mzaliwa wa Madrid, alianza kufundisha Coria mwaka 2008 hadi 2009 akaenda Fuenlabrada kote kama Kocha Msaidizi.

Soma: Magazeti ya  Jumamosi November 06,2021

Mwaka 2010 alikuwa Kocha Mkuu wa Santa Eugenia hadi 2012 akahamia Puertollano hadi 2014 akaenda Getafe B hadi 2015 Getafe A katika La Liga hadi 2016 akahamia Saburtalo Tbilisi ya Georgia hadi 2017.

Kutoka hapo akatua BSU ya China hadi akarejea Hispania na kuwa Kocha Maaidizi wa Real Madrid 2018 hadi 2019 chini ya Kocha Julen Lopetegui na baadaye Santiago Solari ndipo alipojiunga na Al-Qadsia ya Kuwait hadi anahamia Simba SC leo Jumamosi November 11, 2021.

Tags: , ,

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Nijuze Habari WhatsAp Channel
  Nijuze Habari WhatsAp Group
  Nijuze Habari Telegram Channel