MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPA


RATIBA YA ROBO FAINALI CAF CHAMPIONS LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPARATIBA YA NUSU FAINALI CAF CHAMPIONS LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPA


RATIBA YA SIMBA ROBO FAINALI CAF CHAMPIONS LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPA


RATIBA YA YANGA ROBO FAINALI CAF CHAMPIONS LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPA


TIMU 32 Kushiriki Kombe la Dunia la Vilabu 2025

Filed in Michezo by on 25/12/2023 0 Comments

TIMU 32 Kushiriki Kombe la Dunia la Vilabu 2025

TIMU 32 Kushiriki Kombe la Dunia la Vilabu 2025 Marekani

TIMU 32 Kushiriki Kombe la Dunia la Vilabu 2025 Marekani

TIMU 32 Kushiriki Kombe la Dunia la Vilabu 2025, Mwaka 2025 Michuano ya Kombe la Dunia kwa Klabu itafanyika nchini Marekani Kuanzia Juni 15 hadi Julai 13, 2025 mwaka mmoja kabla ya Kombe la Dunia, ambapo Bara la Afrika limepewa nafasi ya kupeleka timu nne (4) Katika Michuano hiyo itakayoshirikisha timu 32.

Bara la Afrika limepewa nafasi nne (4) ambapo nafasi mbili (2) tayari zimechukuliwa na Al Ahly na Wydad Athletic zilizoshinda taji la Ligi ya Mabingwa Afrika katika miaka minne iliyopita.

Timu mbili (ukizitoa Al Ahly na Wydad AC) ambazo zitakusanya alama nyingi katika ranking za CAF baada ya Michuano ya CAF Champions League ya mwaka huu basi zitaungana na Al Ahly na Wydad kushiriki Michuano hiyo.

TIMU 32 Kushiriki Kombe la Dunia la Vilabu 2025

TIMU 32 Kushiriki Kombe la Dunia la Vilabu 2025 Marekani

Lakini pia timu itakayotwaa taji la Ligi ya Mabingwa msimu huu wa 2023/2024 (kama sio Al Ahly, au Wydad Athletic) itakuwa imekata tiketi moja kwa moja ya Kushiriki Michuano hiyo

Mpaka sasa Simba iko Katika nafasi ya tano (5) kwenye ranking ikiwa imekusanya alama 45, Mamelodi Sundowns ikiongoza kwa alama 81 ikifuatiwa na Esperance ya Tunisia yenye alama 75. CR Belouzdad inashika nafasi ya tatu ikiwa na alama 59.

Simba SC yatajwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) kuwania kufuzu Kombe la Dunia la Klabu nchini Marekani (FIFA Club World Cup 2025).

Simba SC yatajwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) kuwania kufuzu Kombe la Dunia la Klabu nchini Marekani (FIFA Club World Cup 2025).

Aidha Simba SC ndiyo Timu pekee Kutoka Afrika Mashariki iliyotajwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) kuwa kwenye Orodha hiyo ya klabu zinazowania kufuzu Kombe la Dunia la Klabu nchini Marekani (FIFA Club World Cup 2025)

TIMU 32 Kushiriki Kombe la Dunia la Vilabu 2025, TIMU 32 Kushiriki Kombe la Dunia la Vilabu 2025 Marekani,Simba SC yatajwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) kuwania kufuzu Kombe la Dunia la Klabu nchini Marekani (FIFA Club World Cup 2025), Simba Kushiriki Kombe la Dunia la Vilabu 2025.


Chelsea na Manchester City ni timu mbili za England zilizofuzu Kushiriki Michuano hiyo baada ya kushinda mataji ya Ligi ya Mabingwa Ulaya siku za karibuni.

Chelsea ilishinda Ubingwa huo 2021 na Manchester City 2023, huku timu zilizopata tiketi ya moja kwa moja Kushiriki Fainali hizo ni zile zilizobeba Ubingwa wa Ulaya ,(UEFA champions League) kuanzia mwaka 2020.

Real Madrid na Bayern Munich zimefuzu Michuano hiyo baada ya kunyakua mataji ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, wakati Paris Saint-Germain, Inter Milan, FC Porto na Benfica zenyewe zimepata nafasi kutokana na pointi zilizovuna kwenye viwango vya Ubora wa Shirikisho la soka Ulaya (UEFA).

Timu 32 Zitashiriki Fainali hizo, ambapo timu mbili kutoka kila taifa itaruhusiwa kushiriki.

Kutakuwa na timu 12 kutoka Ulaya, sita kutoka Amerika Kusini, nne kutoka kila upande, Asia na Afrika na Amerika, wakati moja itatoka huko Oceania na timu ya mwisho ni kutoka nchi mwenyeji, Marekani.

Michuano hiyo itachezwa kila baada ya miaka minne.

Mfumo wa sasa wa Klabu Bingwa utakoma mwaka huu 2023, na Mtindo utakaotumika kwenye Mfumo mpya wa Kombe la Dunia la timu za klabu ni uleule wa kama wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, ambapo timu zitapangwa kwenye Makundi manane yenye timu nne kila moja.

Timu mbili za juu kutoka kwenye kila kundi zitafuzu hatua ya Mtoano.

Tofauti itakayojitokeza ni kwamba kwenye Michuano hiyo itakapofika hatua ya Mtoano hakutakuwa na mechi mbili za nyumbani na ugenini, itapigwa mechi moja tu, ambayo itaamua ni timu gani itasonga raundi inayofuata.

Aidha hakutakuwa na timu itakayoshindania Mshindi wa tatu, kitu ambacho kitachochea michuano hiyo kuwa na upinzani mkali kwa sababu kila timu itahitaji ushindi.

PIA UNAWEZA KUSOMA👇

Tags: , , ,

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Nijuze Habari WhatsAp Channel
  Nijuze Habari WhatsAp Group
  Nijuze Habari Telegram Channel