MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPA


RATIBA YA ROBO FAINALI CAF CHAMPIONS LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPARATIBA YA NUSU FAINALI CAF CHAMPIONS LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPA


RATIBA YA SIMBA ROBO FAINALI CAF CHAMPIONS LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPA


RATIBA YA YANGA ROBO FAINALI CAF CHAMPIONS LEAGUE 2023/24 BOFYA HAPA


WAUGUZI 500 Wanawake Wapata Ajira Saudi Arabia 2023/2024

Filed in Ajira by on 19/12/2023 0 Comments

WAUGUZI 500 Wanawake Wapata Ajira Saudi Arabia 2023/2024

WAUGUZI 500 Wanawake Wapata Ajira Saudi Arabia 2023/2024,Mama Samia amwaga ajira 500 kwa Wauguzi Nje ya Nchi, Wauguzi 500 wa Kike kuajiriwa Saudi Arabia, Neema Wauguzi wa Kike 500 Wapata Ajira Saudi Arabia.

WAUGUZI 500 Wanawake Wapata Ajira Saudi Arabia 2023/2024

WAUGUZI 500 Wanawake Wapata Ajira Saudi Arabia 2023/2024,Mama Samia amwaga ajira 500 kwa Wauguzi Nje ya Nchi, Wauguzi 500 wa Kike kuajiriwa Saudi Arabia, Neema Wauguzi wa Kike 500 Wapata Ajira Saudi Arabia.

Serikali imetangaza neema ya uwepo wa ajira 500 za wauguzi wa kike kuajiriwa na Serikali ya Saudi Arabia mapema mwezi Januari 2024.

Akizungumza na waandishi wa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam, leo (Jana) Desemba 18 2023, Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema kuwa Serikali inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan imeendelea na dhamira yake thabiti ya kuhakikisha watanzania wananufaika na fursa za ajira zinazojitokeza kutokana na mahusiano mazuri yaliyopo baina ya Tanzania na mataifa mbalimbali Duniani.

Mhandisi Luhemeja amesema hivi karibuni mwishoni mwa mwezi Novemba na mwanzoni mwa mwezi Desemba, 2023, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesaini hati mbili za makubaliano ya ushirikiano katika masuala ya kazi na ajira na Serikali ya Saudi Arabia pamoja na Serikali ya Umoja wa Falme za Kiarabu.

Amesema kuwa hati za Mashirikiano zilizosainiwa zinatoa fursa za ajira kwenye mataifa husika kwa kada na sekta zenye kutumia ujuzi wa chini, ujuzi wa kati na ujuzi wa juu.

“Hati hizo zinalenga kuongeza fursa za ajira kwa watanzania kwenye nchi husika na pia kuweka utaratibu rasmi wa kuratibu ajira za watanzania wanaoenda kufanya kazi nje, ili kuhakikisha wajibu na haki za watanzania husika zinalindwa na kuzingatiwa ipasavyo,” amesema Mhandisai Luhemeja.

Amesema watanzania wote wenye sifa na ujuzi uliobainishwa wanataarifiwa kuomba kazi husika kwa kujisajili https://jobs.kazi.go.tz na kutuma wasifu binafsi ((CV) kwa njia ya barua pepe [email protected], ambapo mnwisho wa kutuma maombi ni tarehe 27 Desemba 2024.

WAUGUZI 500 Wanawake Wapata Ajira Saudi Arabia 2023/2024 Download PDF

Mhandisi Luhemeja amesema kuwa kwa watanzania ambao tayari wamejiandikisha wawasilishe wasifu binafsi (CV) zilizohuishwa kwa njia ya barua pepe [email protected].

Katika hatua nyingine, Mhandisi Luhemeja amesema Serikali inaendelea kufanya mashauriano katika hatua mbalimbali na nchi zingine zaidi ya kumi (10) kwa lengo la kuwa na makubaliano ya ushirikiano utakaowezesha watanzania kunufaika na fursa za ajira kwenye nchi husika.

“Tunampongeza sana Rais Samia kwa kuwa chachu ya kufanikiisha mazungumzo haya muhimu. Dhamira yetu ni kuhakikisha Tanzania inakuwa miongoni mwa nchi zinazotoa nguvukazi shindani kufanya kazi sehemu mbalimbali duniani,” amesema Mhandisi Luhemeja.

Ametoa wito kwa watanzania wote wahitimu wa ngazi mbalimbali za elimu na mafunzo katika fani zote wenye nia ya kufanya kazi nje ya nchi kujisajili Kitengo cha Huduama za Ajira (TaESA) kupitia https://jobs.kazi.go.tz na kusisitiza kuwa, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana Ajira na Wenye Ulemavu kupitia TaESA imejipanga kuendelea kutekeleza wajibu muhimu wa kusajili na kuwajengea uwezo watanzania wenye nia na shauku kwenda kufanya kazi nje ya nchi ili kumudu ushindani pamoja na kufanya kazi kwa tija.

Ajira 500 za Wauguzi wa Kike katika Wizara ya Afya, Saudi Arabia Application PDF ‘Angalia Hapa’ Wale ambao tayari wamesajiliwa na TaESA unahitaji tu kutuma CV zako kupitia [email protected]

PIA UNAWEZA KUSOMA👇

Tags: , , , , ,

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Nijuze Habari WhatsAp Channel
  Nijuze Habari WhatsAp Group
  Nijuze Habari Telegram Channel